Vitamani A yawaondolea watoto uoni hafifu

TATIZO la uoni hafifu kwa watoto wachanga limeonekana kupata ufumbuzi na kuhakikisha wajawazito na watoto wanaendelea kupata huduma za afya zilizobora.

Kabla ya kupatikana ufumbuzi wa Matone ya Vitamin A watoto walikuwa wakitokwa na uchafu mweupe machoni na wazazi kuona hali ya kawaida kuwa wanasafisha macho.

Salome Duwaki mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga anasema mtoto wake alipokuwa na umri wa mwezi mmoja alikuwa akimtazama kadri anavyokuwa macho hayana uchafu wowote na anaona.

“Mimi namchunguza mtoto wangu kwa kupitisha mkono wakati mwingine napitisha kitambaa chenye rangi rangi akiwa anakifuatilia nakumgundua anaona”anasema Duwaki.

Kiwilos Mathew mkazi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga anasema macho ya mtoto kuwa na dalili za uchafu huo ni moja kwa moja ni uoni hafifu lakini wazazi walikuwa wakidai mtoto anasafisha macho.

Mathew anasema serikali imejitahidi kuokoa maisha ya watoto na baadhi ya familia haziwezi kutekeleza suala la kumpatia mtoto mboga za majani kwa ufasaha ikaona ije na utaratibu wa matone ya Vitamini A.

Mtaalamu wa magonjwa ya macho kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dk Ntoke Wilson anasema tatizo la uoni hafifu kwa watoto chini ya miaka mitano lililokuwa likisababishwa na ukosefu wa madini ya Vitamin A kwa hivi sasa halipo tena.

Dk Wilson anasema matone ya Vitamin A yamesaidia kuondoa uoni hafifu kwa watoto uliokuwa unasababishwa na ukosefu wa madini ya Vitamin A mwilini.

“Mtoto anapozaliwa huwezi kumbaini kama anatatizo la uoni hafifu kitu ambacho wamekuwa wakikiangalia zaidi kwa mtoto ni masuala mengine lakini kuhusu uonaji wake huendelea kuchunguzwa taratibu katika makuzi yake ”anasema Dk Wilson.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Yudas Ndungile anasema hivi sasa hakuna mtoto aliye chini ya umri wa miaka mitano mwenye uoni hafifu.

Dk Ndungile anasema wajawazito na watoto waliochini ya umri wa miaka mitano wamekuwa wakilindwa kwa namna yoyote ile ili waweze kutimiza chanjo au matone ya Vitamin A yanayohitajika kwao.

pharmacy

Dkt Ngungule anasema mjamzito anapokosa lishe kunauwezekano wa kuzaa mtoto mgongo wazi na akikosa vitamin A anakuwa na upofu sanjari na kukosa vitamin C anakuwa akitokwa na damu mdomoni wakati wa kupiga mswaki..

Ofisa lishe Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mankiligo Said anasema utafiti mdogo uliofanyika mwaka 2019 kwa Mkoa wa Shinyanga baada ya kutolewa kwa matone ya Vitaminia A hakuna mtoto aliyebainika kuwa na uoni hafifu.

‘Watoto ambao wamekuwa wakipatiwa matone ya vitamini A ni wale wenye umri wa kuanzia miezi sita hadi miezi 59 lengo la kuwapatia matone ya Vitamini A ni kuondokana na uoni hafifu , utapiamlo pamoja na kupimwa hali ya lishe”anasema Said.

Ofisa lishe Mkoa wa Shinyanga Hamis Yusuph anasema watoto 323,428 walipatiwa matone ya vitamin A kwa mwezi Desemba mwaka 2023 kati ya watoto 296,656 waliokuwa wamelengwa.

Yusuph anasema mjamzito anashauriwa kunywa matone ya Vitamini A mara baada ya kujifungua au ndani ya kipindi cha wiki nane za kujifungua kama atakavyoshauriwa na mtoa huduma na itasaidia kujenga kinga ya mwili na mtoto wake.

Josephat Mussa mwakilishi wa shirika la Word Division kanda ya Tabora na Shinyanga lililokuwa na mradi wa Enrich mkoani Shinyanga kwenye baadhi ya wilaya walikuwa wakitekeleza kwa kutoa elimu ya lishe na ulimaji wa mbogamboga na viazi lishe vyenye madini ya vitamin A.

Shirika la Nutrition International la nchini Canada limetoa vidonge vya matone ya vitamin A milioni 22 vyenye thamani ya Sh bilioni 100.3 kwaajili ya kuwapatia matone hayo watoto milioni 11 walio chini ya miaka mitano kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Shirika lilimkabidhi Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk Jakaya Kikwete ambaye mjumbe wa bodi ya menejimenti nchini wa shirika hilo.

Dk Kikwete anasema matone hayo atayakabidhi serikalini yatatumika mara mbili kwa mwaka mmoja kwa mwezi Juni na Disemba mwaka 2024.

“Faida ya vitamini A ni kuimarisha afya ya macho na kuongeza kinga ya mwili kwa mtoto hivyo ni muhimu kwa wazazi kuhakikisha watoto wanapatiwa matone haya anasema Dk Kikwete.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel anasema Vidonge vya matone ya Vitamini A vitasaidia kuongeza kinga ya Mwili na kuimarisha afya ya macho kwa watoto walio na umri chini ya miaka tano.

Mollel anasema lishe ya mtoto inaanza siku mimba inatungwa na wakati ujauzito ili kusaidia kuimarisha ubongo wa Mtoto.

Serikali ya Tanzania kupitia sera ya afya ya mwaka 2007 imewekeza kuboresha uhai wa mtoto kupitia huduma bure za afya kwa wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Katika toleo la kitabu cha programu jumuishi ya Taifa ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) inaeleza upatikanaji wa nyongeza ya virutubishi havitoshi hapa nchini ikiwa ni asilimia 63.7 ya watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 59 ndiyo waliopata nyongeza ya vitamin A.

Mshauri kutoka shirika la watoto duniani UNICEF Kanda ya Mashariki mwa Afrika na Kusini Dk Oliver petrovic anapongeza juhudi za nchi kuanzisha msingi imara ikiwemo Afya kwa kila mtoto kukuza mtaji wa ubinadamu.

Habari Zifananazo

Back to top button