DODOMA; Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, Mhandisi Ezra Chiwelesa ameiomba serikali kuharakisha utoaji wa vitambulisho vya uraia (NIDA) kwa lengo la kuwasaidia wananchi wanaoishi maeneo ya mipakani.
Akichangia bajeti ya makadirio ya fedha ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka 2024/2025,Mhandisi Chiwelesa amesema changamoto kubwa iliyokuwepo wakazi wengi wa maeneo hayo wamekuwa wakipata shida pale wanapotakiwa kuthibitisha uraia wao.
Amesema changamoto nyingine maafisa uhamiaji wa eneo hilo wameshindwa kutoa msaada wa huduma hiyo huku wakiendelea kudhihaki kuwasaidia Watanzania.
“Watu wanaenda pale kuomba hata fomu tu kujaza, akimuona anamwambia wewe si Mtanzania anamfukuza unataja jina anakwambia wewe si Mtanzania sasa utanzania wa mtu unamuangalia kwa jina ama kwa sura au umpe fomu ajaze halafu umfanyie vetting ndio ujue ni Mtanzania au sio Mtanzania, “ amesema Chiwelesa