Vitendo vya unyanyasaji 593 vyaripotiwa Arusha

SERIKALI na wadau wa masuala ya kijinsia wakati wakiendelea kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia, katika Halmashauri ya Arusha iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha kumeripotiwa matukio 593 ya vitendo vya ukatili wa kijinsia huku ukatili wa kingono ukiongoza kwa kuwa na matukio 272 kati ya mwezi Julai 2023 hadi Januari 2024.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha, Mwanasheria Mkuu wa Halmashauri hiyo,  Monica Mwailolo wakati akitoa taarifa hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo katika halmashauri hiyo yamefanyika katika shule ya Sekondari ya Lengijave amesema katika takwimu hizo matukio 220 ni  ukatili wa mwili ,97 ukatili wa kingono ,272 ukatilii wa kisaikolijia pamoja na matukio manne ambayo ni  ukatili wa kiuchumi .

Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya, Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Arumeru, Frola Msilu amesema maadhimisho hayo yatumike kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili ikiwemo kuwahimiza wanawake kujihusisha katika shughuli za uchumi .

Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Arumeru, ASP Frimina Massao amesema  wakina mama wanapaswa kuwa mstari wa mbele kutokomeza ukatili na unyanyasaji wa kijinsia lengo ni kuwasaidia watoto na vijana waweze kutimiza ndoto zao za baadaye.

Habari Zifananazo

Back to top button