Vitenge 16,000 vyadakwa kwenye jahazi

JESHI la Polisi mkoani Tanga limekamata vitenge doti 16,000 vilivyoingizwa katika mkoa huo kwa magendo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omar Mgumba alisema walikamata boti iliyokuwa na mali ya magendo ikiwa inatoka Unguja na kuingia katika eneo la bahari la mkoa huo.

“Tuliweza kukamata jahazi Katika eneo la Moa wilayani Mkinga ikiwa na mali za magendo mabalo 170 yenye jumla ya vitenge 16,000 vikiwa vinasafishwa kuingia mkoani hapa huku kukiwa hakuna nyaraka zinazoonyesha mzigo ulipotoka wala unapokwenda”alisema Mgumba.

Advertisement

Aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, katika oparesheni maalumu pia walikamata dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 430 nyuma ya nyumba ya mshukiwa wa biashara hiyo katika eneo la Sahare jijini Tanga.

Mgumba alisema oparesheni hiyo imelenga kudhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya , biashara za magendo na wahamiaji haramu katika mkoa huo.