Viwanja maonesho ya kilimo kuboreshwa

Waziri Bashe

Wizara ya kilimo imepanga kuboresha viwanja vya maonesho ya kilimo ili kuendana na hadhi ya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ikiwa ni fursa ya kutangaza kilimo na bidhaa zake kimataifa.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe  ameeleza hayo leo Jumatatu Mei 8, 2023 wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara katika mwaka wa fedha  2023/2024.

Waziri Bashe amevitaja viwanja hivyo kuwa ni kuwa kiwanja cha  maonesho ya kilimo cha  John Mwakangale  cha mkoani Mbeya na kiwanja cha Nzuguni, Dodoma.

Advertisement

Amesema mpango huo utahusisha usanifu wa viwanja hivyo ili kukarabati na kujenga miundombinu ya viwanja hivyo na  pia kujenga Makumbusho ya Kilimo ( Tanzania Agricultural Museum), ili kukidhi hadhi ya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa.

Bashe amesema  katika kilele cha Maonesho ya Kilimo (Nanenane) mwaka 2022, Rais Samia Suluhu Hassan alielekeza kuanzisha Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Tanzania International Agriculture Trade Show) badala ya kutumia utaratibu uliozoeleka.

Aidha, Rais Samia alielekeza mabadiliko hayo yaanzie na ujenzi wa miundombinu katika kiwanja cha Maonesho cha John Mwakangale (Mbeya) kilichopo katika ukanda wa Nyanda za Juu Kusini, ambapo kuna uzalishaji mkubwa wa mazao.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *