Viwanja vya Mkapa, Uhuru kufungwa hadi Oktoba 24

WIZARA ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema imepokea taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) za kuufungia uwanja wa Uhuru kutokana na kutokidhi vigezo vya kikanuni kutumika katika michezo ya Ligi Kuu.

Wizara imeeleza kuwa awali wakati viwanja vya Benjamini Mkapa na Uhuru vikiwa kwenye ukarabati, ilipokea maombi baadhi ya klabu kutumia viwanja hivyo, hata hivyo kutokana na mahitaji makubwa ya michezo ya ndani na kimataifa wizara iliridhia hilo.

“Hata hivyo, kutokana na maombi ya timu zinazocheza Ligi Kuu na uhitaji mkubwa wa viwanja hivyo kwa ajili ya michuano ya Kimataifa, Wizara iliridhia ombi la kuendelea kutumika kwa viwanja hivyo wakati ukarabati ukiendelea, kazi ya ukarabati mkubwa inaendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Uhuru upo mbioni kuanza.” Imeeleza taarifa,”

“Kwakuwa ni muhimu kuzingatia kanuni zinazosimamia Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa, Wizara inatangaza kuvifunga viwanja vya Benjamin Mkapa na Uhuru mpaka hapo ukarabati utakapokamilika Oktoba, 2024.”

Wizara imeeleza kuwa timu zilizoomba kutumia viwanja hivyo kama viwanja vyao vya nyumbani zinapaswa kutafuta viwanja vingine.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button