Vyama vya siasa 18 vyaomba usajili

MSAJILI wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi amesema vyama vipya vya siasa 18 vimeomba usajili ambapo utaanza kutekelezwa baada ya kuhitimishwa zoezi la uhakiki wa vyama vilivyopo.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kikao kazi na viongozi wa vyama vya siasa nchini ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye uhakiki huo Mutungi amesema kwamba hawezi kusajili vyama vipya kabla ya kufanyika uhakiki katika vyama vilivyopo.

Aidha jaji Mutungi amesema wanaotaka kufuta hati chafu ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa kuhakikisha vyama vinakuwa na wataalamu wa fedha ambao watakuwa wanafanya shughuli kwa kuzingatia weledi.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba ameipongeza ofisi hiyo kwa kuandaa mkutano huo ambao ameeleza utasaidia kutoa uelewa na namna ya kuendesha vyama vyao.

Shughuli ya uhakiki huo inatarajiwa kuanzia Julai 20 mwaka huu ambapo ofisi ya Msajili inawajibika kulinda uhai wa vyama hivyo kwa kuvikagua na kubainisha mapungufu yanayojitokeza kisha kutoa muda kwa utekelezaji.

Habari Zifananazo

Back to top button