Vyombo vya habari vyatakiwa kufuata sheria,kanuni za uchaguzi

DAR ES SALAAM :MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Jacobs Mwambegele, amewataka wanahabari kote nchini kutumia taaluma yao kwa weledi katika kipindi cha kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ili kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu kwa amani na utulivu.