Vyuo vinavyotoa elimu ya udereva kukaguliwa

Vyuo vinavyotoa elimu ya udereva kukaguliwa

SERIKALI imesema itakagua vyuo vyote nchini vinavyotoa elimu ya udereva kuona kama vina sifa zinazostahili.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alisema hayo Dar es Salaam jana katika kikao kilichowakutanisha wasafirishaji na wamiliki wa magari na wakuu wa usalama barabarani kwa Tanzania Bara na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IJP), Camillius Wambura.

Masauni alisema yapo maeneo matatu ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi na serikali, lakini pia yapo yale yanayowahusu wamiliki na wasafirishaji.

Advertisement

Masauni alisema suala la sheria ya usalama barabarani kuwa ni ya muda mrefu pamoja na utolewaji wa stika za barabarani bila utaratibu ni suala litakalofuatiliwa.

Aliwataka madereva kutumia fursa ya kujisajili na wamiliki wasitumie mwanya uliopo kwa kuwatumia madereva wasiojisajili.

Masauni aliwataka wamiliki wa vyombo hivyo kutekeleza sheria iliyopo kwa sasa na kuangalia vyema suala la kuajiri madereva wakitizama zaidi dhamana wanayowapa pamoja na kujali uhai wa abiria.

Awali IJP Wambura alisema wapo waendesha magari wengi kuliko madereva na wote hao wana leseni.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *