Vyuo vya kodi vyapewa rungu udhibiti wa mapato ya serikali

DAR ES SALAAM: ILI kuisadia Serikali katika mapambano ya udhibiti wa mapato ni wajibu kwa vyuo vya kodi na fedha kuwajenga wanafunzi sio tu kitaaluma ila pia kimaadili, uzalendo, na kuepukana na vitendo vya rushwa.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Profesa Isaya Jairo katika mkutano wa ITA na waandishi wa habari kuelekea mahafali ya 16 ya chuo hicho kilicho chini ya Mamlaka ya Mapato nchini TRA.

“Ili kuwapa wanafunzi uelewa mpana zaidi wa kimaadili na uwajibikaji, tuliwahi kuwaita masheikh na wachungaji kuzungumza na walimu darajani,” amesema mkuu huyo wa chuo.

Amesemakatika mahafali ya ITA, Novemba 24, 2023 jumla ya wanafunzi 508 wanahitimu. Kati yao, 293 ni wanaume na 215 ni wanawake.

“ITA inajivunia mafanikio mengi katika utekelezaji wa Mpango Mkuu wa tano wa Chuo ambao umejikita zaidi katika kutoa mafunzo kwa njia za kisasa za kidijitali,” amesema Prof. Jairo.

Amesema mgeni rasmi katika mahafali hayo anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, ambapo atawatunuku wanafunzi vyeti vya Stashahada, Shahada na Shahada ya uzamili.

“Atatoa zawadi kwa wahitimu na wanafunzi wanaoendelea na masomo na waliofanya vizuri zaidi katika mwaka wa masomo 2022-24. Amesema Profesa Jairo.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button