Vyuo vya utumishi kuboreshwa

SERIKALI imesema kuwa imejipanga kuboresha vyuo vya utumishi  wa umma nchini viweze kuendana na mabadiliko yaliyopo, ikiwemo kutoa wahitimu watakaoweza kutoa huduma bora kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa na Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama wakati alipokuwa akipokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Tanga kabla ya ziara yake ya kutembelea chuo cha utumishi wa umma kilichopo mkoani humo.

Amesema kuwa vyuo hivyo vimekuwa na mchango mkubwa katika ustawi wa utumishi wa umma hapa nchini, hivyo umefika wakati wa kuvifanyia maboresho, ili viweze kuendelea kunoa watumishi.

“Rasilimali watu ni kitu muhimu katika Maendeleo ya sekta ya utumishi wa umma, hivyo ni muhimu kuvitazama vyuo vyetu viweze kutoa watu wenye kukidhi viwango, ambayo vitasababisha kuwepo na huduma bora inayotakiwa na wananchi,”amesema Waziri Mhagama.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba  ameishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha maslahi ya watumishi wa umma, ikiwa ni pamoja na kulipa malimbikizo ya mshahara.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x