Waagizwa kutumia Tehama kuendana na mabadiliko

BODI ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala imeagizwa kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), katika utendaji kazi wake ili kuendana na mabadiliko ya dunia.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba ameagiza hayo alipofungua mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa kampuni za waendesha ghala, wasimamizi wa ghala, meneja dhamana pamoja na washiriki binafsi yaliyofanyika katika Uwanja wa Maonesho ya Sabasaba mkoani Dar es Salaam.

Amesema hilo likitekelezeka litachochea utoaji wa huduma bora kwa wadau wote, pia alisema mafunzo hayo yataongeza heshima kwa watendaji wa ghala.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Stakabadhi za Ghala, Asangye Bangu amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza tija katika ufanyaji kazi kwa kuzingatia sheria.

“Bodi ya Udhibiti na Usimamizi wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala imejipanga kuona ambavyo itatekeleza shughuli zake za kiserikali ikiwa ni pamoja na kuingiza bidhaa mbalimbali kadri sheria ilivyoruhusu kufanya hivyo,” amesema.

Amesema alipofanya ukaguzi alibaini changamoto mbalimbali kwenye maghala ambazo kupitia mafunzo hayo watapata uwezo wa kiutendaji.

Habari Zifananazo

Back to top button