DAR ES SALAAM: UKIUKWAJI wa taratibu na kanuni za usajili wa wanachama na uwasilishaji wa michango yao kutoka kwa waajiri na kuwasilisha michango iliyo chini ya mshahara halisi wa mtumishi, umekuwa mojawapo ya changamoto kubwa kwa mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii NSSF,katika kufikia malengo yake ya kutoa huduma bora kwa jamii.
Hayo yamesemwa leo Septemba 25,2023 na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba katika mkutano wa Wahariri na waandishi, wa Vyombo vya habari uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema wapo waajiri ambao hawatoi mikataba ya ajira kwa watumishi wao, hivyo wanaandikisha wanachama wachache kuliko waliopo kwenye ajira.
Mshomba amesema kuanzia Machi 1, 2023 hadi Juni 30, mali zote za mfuko zimeongezeka kutoka Sh.
bilioni 2 hadi kufikia Sh. bilioni 8, ikiwa ni ongezeko la asilimia 55 zikichangiwa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa mapato yanayotokana na michango, uwekezaji.
Kuhusu utekelezaji wa miradi iliyokuwa imesimama, NSSF imetatua changamoto hiyo na utekelezaji wa miradi inaendelea, ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha sukari Mkulazi ambapo hadi kufikia Juni 30, 2023 utekelezaji wake umefikia asilimia 93 na utakamilika na kuanza uzalishaji wa sukari mwishoni mwa mwezi oktoba.
Akitoa salamu kwa niaba ya jukwaa la wahariri TEF Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Deodatus Balile amependekeza elimu itolewe zaidi kwa waajiri juu ya umuhimu wa kupeleka michango ya watumishi wao kwa wakati NSSF.
Comments are closed.