Waandamaji DR Congo, polisi watumia mabovu ya machozi

POLISI nchini DR Congo wamelazimika kutumia mabovu ya machozi kutawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa upinzani katika mji mkuu Kinshasa wanaotaka kurudiwa kwa uchaguzi wa rais na wabunge uliofanyika wiki iliyopita.

Wapinzani watano wa Rais Felix Tshisekedi walitoa wito kwa wafuasi wao kuungana na kupinga uchaguzi huo, ambao wanasema ulikuwa wa udanganyifu na unapaswa kufutwa.

Waliapa kuendelea hata baada ya serikali kupiga marufuku maandamano hayo Jumanne, wakisema yalilenga kuhujumu utendakazi wa tume ya kitaifa ya uchaguzi.

Polisi walizingira makao makuu ya mmoja wa wapinzani wakuu Martin Fayulu, ambapo waandamanaji walikusudiwa kukusanyika. Baadhi ya waandamanaji walijaribu kufunga barabara kwa kutumia matairi yanayowaka moto huku wengine wakiwarushia mawe polisi.

Habari Zifananazo

Back to top button