Waandamana kupinga ushoga
wataka serikali kukagua vyakula kutoka nje
WAUMINI wa dini ya Kiislamu mkoani Tanga leo wameandamana kupinga ndoa za jinsia moja.
Maandamano hayo ambayo yamepokelewa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa yamelenga katika kuiunga mkono serikali katika vita dhidi ya vitendo hivyo.
Akiongea Shekhe wa Mkoa wa Tanga Jumaa Luwuchu amesema kuwa viongozi wa dini wanajukumu la kuiunga mkono serikali na kuisemea katika mambo ambayo yanahusisha jamii moja kwa moja.
“Kuna mambo serikali inapata kigugumizi kuyazungumza hivyo sisi kama viongozi wa dini ni jukumu letu kuisema serikali katika mambo magumu kama hilo la kupinga mapenzi ya jinsia moja”amesema Shk huyo.
Aidha katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga Suleiman Mzee ameitaka serikali kuchunguza vyakula na dawa zinazotoka ili kubaini kama yanaviambata vya homoni za ushoga na kuviharibu kabla ya kufika kwa watumiaji.
Hata hivyo, Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amewataka wananchi wote kuwa mabalozi katika kupiga vita vitendo hivyo kwani vinachangia kuharibu nguvu kazi ya Taifa