Waandamana wakihofia sheria ya Urusi

POLISI nchini Georgia imewafyatulia mabomu ya kutoa machozi maelfu ya waandamanaji walipokuwa wakiandamana kwa siku ya pili mfululizo kupinga sheria inayofanana na ile iliyowekwa Urusi kuwanyamazisha wakosoaji wa serikali.

Mwandishi mmoja wa shirika la habari la Ufaransa AFP ameshuhudia makundi makubwa ya watu waliokuwa wamekusanyika nje ya majengo ya bunge katikati mwa mji mkuu Tblisi wakiwa wamebeba bendera za Umoja wa Ulaya na Georgia wakipinga kile walichokiita “sheria ya Urusi” nchini humo.

Mswada wa sheria hiyo uliidhinishwa na wabunge wiki hii uliposomwa bungeni kwa mara ya kwanza. Mswada huo iwapo utapitishwa na kuwa sheria, utahitaji vyombo vya habari na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayopokea zaidi ya asilimia 20 ya ufadhili wao kutoka mataifa ya kigeni, kujiandikisha kama “mawakala wa ushawishi wa kigeni.”

Habari Zifananazo

Back to top button