Waandishi waomba kupata taarifa za SADC kwa wakati
WAANDISHI wa habari wameomba kushirikishwa kila hatua yanayofanyika katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ili kupata uwanda mpana wakuwajuza wananchi kuhusu mambo mbalimbali katika jumuiya hiyo.
Wito huo umetolewa na wandishi wa habari wa vyombo tofauti waliposhiriki semina ya kuwajengea uwezo kuhusu Jumuiya hiyo iliyoandaliwa na Mtandao wa wakulima wa Afrika Mashariki na nchi za Kusini mwa Afrika (ESAFF) kwa kushirikiana na Kituo cha Malengo ya Maendeleo Endelevu Afrika (SDGCA).
Semina hizo ni moja ya utekelezaji wa Mradi wa Mpango Jumuishi wa Kujenga Uwezo wa Kitaasisi (IICB) kwa Sekretarieti ya SADC na Wadau wa Kitaifa kwa kushirikiana na wadau wake katika kufikia ahadi za kikanda hususan, Mpango Elekezi wa Kikanda wa Maendeleo (RISDP) – (2020-2030) na Dira ya 2050 ya SADC.
Kati ya waliotoa maoni na mtazamo juu ya Jumuiya hiyo ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) Salome Kitomari alisema katika kuhabarisha huko kwa sasa kinachofanywa ni waandishi kutakiwa wakati kunapokuwa na matukio kama vile ujio wa viongozi na mikutano mbalimbali mikubwa inayofanyika.
Philipo Mhava kutoka redio Clouds,alisema hata lugha ya Kiswahili imekuwa ngumu kutumika katika utoaji taarifa unazohusu Jumuiya hiyo na kuwatenga hata watanzania wakawaida kuifahamu na kufuatilia yanayoendelea ndani ya Jumuiya hiyo.
Kwa upande wa Mratibu wa ESAFF, Joe Mzinga,alisema malengo ni kuhakikisha vyombo vya habari vinajengewa uwezo na kuwezeshwa kuweza kutoa habari zaidi kuhusu SADC.
Mradi huo umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya na unatekelezwa katika nchi za Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe,