Waandishi wapewa ‘dawa’ kukwepa rushwa ya ngono

DSM; MKURUGENZI  Mstaafu wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Dk. Ananilea Nkya amesema rushwa ya ngono inaweza kukomeshwa na waandishi wa habari wanawake wenyewe kwa kuinuka na kufanya kazi kwa bidi, huku wakijiwekea malengo ya kufika mbali zaidi kutaaluma.

Dk Rose ameyasema hayo, jijini Dar es Salaam, katika kikao cha majadiliano kilichoandaliwa na TAMWA kwa kushirikiana na Mfuko wa Udhamini wa Wanawake Tanzania (WFT-T) kupitia mradi wa kuangazia rushwa ya ngono kwa wanahabari wanawake

“Ni muhimu kuhakikisha unafanya kazi kwa bidii na kuacha uzembe ukiwa kazini, weka malengo yako binafsi na uweze kuyafikia, heshimu kila mtu, andika stori nyingi hadi bosi wako kazini ashangae, ukifanya hayo heshima yako itakua kazini na rushwa ya ngono itakupitia mbali,” amesema Dk Nkya .

Habari Zifananazo

Back to top button