MKURUGENZI wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohammed Janabi amesema watu watano wamejitokeza kujisajili kupata huduma ya kurekebisha maumbo huku akisema zoezi hilo linalenga matibabu.
Prof Janabi amesema hadi sasa ni mgonjwa mmoja ameomba kufanyiwa huduma hiyo kwa ajili ya urembo ambapo awamu hii watafanya kwa watu 6 hadi 10.
“Tunategemea wahitaji zaidi kwa mara ya kwanza hatuwezi kufanya wengi na muda ni mdogo tutaona kwasababu tutafanya nyingine na wenzetu wa Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka,”ameeleza Prof Janabi.
Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Muhimbili-Mloganzila Dk Erick Muhumba ameiambia HabariLEO kuwa wanafanya upasuaji wa aina mbili ambao wa kwanza ni upasuaji wa kupunguza uzito na upasuaji rekebishi.
Ameainisha kuwa gharama za upasuji zinatofautiana kuanzia Sh milioni 15 hadi Sh milioni 25 ambapo inategemea na mtu na aina ya upasuaji na kadiri wanavyotofautiana na gharama zinatofautiana hata kama upasuaji ni mmoja.
“Hayo ni matibabu kwasababu kuna watu wana kisukari shida yake ni unene anapofanya upasuaji inamsaidia ,lakini pia kupunguza unene inalinda ,kuna magonjwa moyo,presha na figo na mengine yanalinda kiasi kubwa ni matibabu.