Waarabu wamganda Bruno Fernandez

JIDDAH, Saudi Arabia: KLABU ya Al-Hilal ya nchini Saudi Arabia imepanga kumnunua nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes msimu wa majira ya joto baada ya kiungo huyo kukataa ofa nono katika dirisha dogo la mwezi Januari.

Chombo kimoja cha habari nchini Ureno kimeripoti kuwa Fernandes alipokea ofa hiyo kutoka Saudi Pro League lakini kiungo huyo wa kati wa Ureno “hakujibu vizuri” ofa hiyo.

Licha ya Fernandes kuikataa Al-Hilal, hamu yao kwa kiungo huyo bado haijapungua, na wanakusudia kutumia mbinu nyingine za ziada katika msimu wa majira ya joto.

Baada ya kujiunga na Manchester United ya England kwa takriban pauni milioni 68 mnamo Januari 2020, Bruno Fernandes anahisi bado ana mengi ya kutimiza katika klabu hiyo ya Jjiji la Manchester, England.

Habari Zifananazo

Back to top button