Waasi washambulia meli Yemen

TEL AVIV, ISRAEL: Meli iliyokuwa ikisafiri Kusini mwa Bahari Nyekundu imeshambuliwa na ndege inayoshukiwa kuwa ya waasi wa Houthi kutoka Yemen mapema leo, mamlaka imesema.

Shambulio hilo limetokea Magharibi mwa Bandari ya Yemen ya Hodeida, na kombora hilo lilisababisha uharibifu mdogo kwenye madirisha ya meli, oparesheni ya biashara ya Bahari ya Uingereza ya jeshi la Uingereza ilisema katika taarifa yake.

Kampuni ya ulinzi ya kibinafsi ya Ambrey imesema inatambua kutokea kwa tukio hilo na kusema meli hiyo ilikuwa meli ya mizigo yenye bendera ya Barbados, inayomilikiwa na Uingereza. Hakuna mtu aliyejeruhiwa kwenye meli, ambayo ilipata “uharibifu mdogo,” kampuni hiyo ilisema.

Baadaye, msemaji wa jeshi la Houthi wanaoungwa mkono na Iran, Brigedia Jenerali Yahya Saree, alidai katika taarifa yake kwamba vikosi vya waasi vilishambulia meli mbili tofauti, moja ya Marekani na nyingine ya Uingereza, katika Bahari Nyekundu. Hakutoa ushahidi wowote kuunga mkono dai hilo.

Moja ya meli ambazo Wahouthi walidai kushambulia ni Morning Tide, kulingana na maelezo yaliyotolewa na Ambrey.

Mmiliki wa Morning Tide, kampuni ya Uingereza ya Furadino Shipping, aliiambia The Associated Press hakuna mtu aliyejeruhiwa katika shambulio hilo na meli ilikuwa ikiendelea kuelekea Singapore.

Tangu Novemba, waasi wamekuwa wakilenga mara kwa mara meli katika Bahari Nyekundu juu ya mashambulizi ya Israeli huko Gaza dhidi ya Hamas.

Imeelezwa mara kadhaa wamelenga meli zilizo na uhusiano mbaya au zisizo wazi na Israeli, na kuhatarisha meli katika njia kuu ya biashara kati ya Asia, Mashariki ya Kati na Ulaya.

Habari Zifananazo

Back to top button