Wababe 20 kushiriki kombe la Angeline Mwanza

TIMU 20 kutoka Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza zinatarajia kushiriki mashindano ya Kombe la Angeline Jimbo 2023.

Kuelekea mashindano hayo, timu zote shiriki zimepatiwa jezi seti moja na mipira miwili.

Timu zinazotarajia kushiriki mashindano hayo yatakaoanza Jumamosi hii ni Kundi A litakalochezwa katika uwanja wa Baptist ni kata za Kirumba, Ibungiro, Kitangiri, Pasiansi, Nyamanaro.

Kundi B michezo yao itachezwa katika uwanja wa Sabasaba ni kata Buzuruga, Nyasaka, Kawekamo, Kiseke na Ilemela.

Kundi C katika uwanja wa shule ya Buswelu sekondari itashirikisha kata za Buswelu, Mecco, Nyakato, Kahama na Nyamhongolo.

Kundi D litashirikisha timu za Bugogwa, Sangabuye, Shibula, Bezi na Kayenze.

Mbunge wa jimbo la Ilemela, Dk Angeline Mabula amesema mshindi wa mashindano hayo atapokea fedha taslimu Sh milioni 2.5 pamoja na kikombe huku nafasi ya pili atapokea Sh milioni 2.

Amesema nafasi ya tatu atapokea Sh milioni 1.5 huku nafasi ya nne atapokea Sh milioni 1.

Amesema kwa upande wa timu timu yenye nidhamu na timu ya mashabiki bora zote zitapokea shilingi 500,000/- kwa kila timu.

Amesema mwamuzi bora na mwandishi bora watapokea Sh 300,000 huku mchezaji bora atapokea shilingi 200,000/-.

Naye mratibu wa mashindano hayo Almas Moshi amewaomba wadau na wapenzi wa soka mkoani Mwanza wajitokeze kwa wingi wakati wa mashindano hayo.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button