Wabunge 19 viti maalum hatuwatambui

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema hawawatambui wabunge 19 waliowapachika jina la wabunge wa Covid kwa kile walichosisitiza kuwa hawakupatikana kwa njia halali.

Mbowe ameyasema hayo leo Machi 8, 2023 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwenye kongamano maalum la wanawake wa Chadema.

Amesema, kitendo cha kupeleka Wabunge 19 ambao hawakutokana na maamuzi ya  ndani ya chama chao ni uvunjaji wa Katiba, ni uvunjaji wa maadili na kitendo hicho ni uhuni ambao hauwezi kuvumiliwa na mtu yeyote”.

Advertisement

“Taasisi kama Bunge ambayo inapaswa kutunga sheria lakini inashiriki katika haya, pamoja na kuwa Spika anafahamu hakuna zuio lolote la wao kuwepo ndani ya Bunge lakini wameendelea kuwepo humo”.

“Wale wanajiwakilisha wao wenyewe na familia zao hawamwakilishi mtu yeyote mule bungeni”

“Mheshimiwa Rais with due respect (kwa heshima kubwa) nakuomba uhurumie zile kodi za Wananchi ambazo mnawalipa wale Wabunge na hawamwakilishi mtu yeyote mule.” Amesema Mbowe

Hata hivyo, akijibu ombi hilo Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa suala la wabunge hao lipo mahakamani na si vema yeye kuingilia muhimili wa mahakama.

“Tuachie mkondo ule uendelee ..tutizame mbele yanayokuja si raisi mimi kutia mkono.