Wabunge Afrika Kusini wapiga kura kusitisha uhusiano na Israel

WABUNGE wa Afrika Kusini wamepiga kura Jumanne kuunga mkono kufungwa kwa ubalozi wa Israel mjini Pretoria na kusimamisha uhusiano wote wa kidiplomasia hadi makubaliano ya kusitisha mapigano yatakapokubaliwa katika vita vyake na Hamas.

Hoja hiyo ilipita kwa kura 248 za ndio na kura 91 za kupinga.

Azimio hilo kwa kiasi kikubwa ni la kiishara kwani itakuwa juu ya s
Serikali ya Rais Cyril Ramaphosa iwapo itatekeleza; msemaji wa ofisi ya rais alisema.

Ramaphosa “anakumbuka na kuthamini” mwongozo wa bunge kuhusu uhusiano wa kidiplomasia wa Afrika Kusini na Israel, hasa kuhusu hadhi ya ubalozi.

Azimio hilo la bunge lililetwa na chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF) wiki iliyopita wakati chama tawala cha African National Congress kilipoahidi kuliunga mkono.

1 comments

Comments are closed.