‘Wabunge hawajapandishwa mshahara’

DODOMA: OFISI ya Bunge, kitengo cha mawasiliano imekanusha taarifa za wabunge kuongezewa mishahara kutoka Sh milioni 13 hadi 18.

Taarifa iliyotolewa leo na ofisi hiyo imefafanua kuwa taarifa za wabunge kuongezewa mishahara ni uzushi.

“Tunapenda kuujulisha umma kwamba madai hayo ni uzushi, na upotoshaji kwakuwa hakuna mbunge aliyeongezewa mshahara,” imeeleza taarifa hiyo.

Advertisement

Machi 22, 2024 Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe akiwa Babati mkoani Manyara alisema wabunge wameongezewa mishahara kutoka Sh milioni 13 hadi 18.