Wabunge: Mwigulu utachinja miguu au shingo?

'hatutaki swaga za kufungia biashara, nyongeza kodi ya saruji'

WABUNGE wamemtaka Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba kuchukua maamuzi magumu kwa kupandisha ushuru kwenye mafuta ya kula yanayotoka nje huku wakimtaka kuacha kufungia biashara za watu kwa kisingizio cha kodi.

Wakizungumza Bungeni leo, Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku ‘Musukuma’ na Mbunge wa Mufindi Kusini David Kihenzile walisema wafanyabiashara wa ndani wanatakiwa kuboreshewa biashara zao ili kutoa wigo wa kukusanya mapato zaidi ya serikali na sio kutishwa, kunyanyaswa na kufungiwa biashara zao.

Akizungumza Kihenzile amesema “Kuboresha biashara; tunahitaji kuongeza walipa kodi ‘tax base’ iongezeke, lakini mkakati wa kuwajali wafanyabishara hauridhishi.”Amesema Kihenzile na kuongeza

“Wizara ya fedha mtusaidie acheni kukimbilia kufungia watu maduka, wale ni watanzania wenzetu kaeni nao chini mzungumze nao, muwaelimishe, hamkupelekwa shule ili mje mnyanyase na kudhalilisha wafanyabiashara.’Amesema

Kwa upande wa Musuma amesema “Suala la mafuta ya kula Mwigulu unawakati mgumu sana chukua maamuzi, mimi nilitegemea utakuja hapa na taarifa umepandisha ushuru wa mafuta yanayotoka nje ili shemeji zangu wa Singida maelfu na maelfu wanaoshinda Barabarani na vidumu, mafuta yao yaende kwa bei kubwa.

“Hivi kweli watu walivyolima vile shemeji zangu wa Singida tushushe tena mafuta, leo kadondokea kwa sheikh wapiga kura wako wanakusikiliza utaangalia uchinje kuanzia mguuni au shingoni, tunataka kuona zao hili halishuki thamani na wakulima hawakatishwi tamaa.”Amesema

Akizungumzia saruji Musuma amesema “Sisi tunaokaa kijijini nyumba zipo hoi, tunataka na sisi tuwe na nyumba za mabati kama Dar es Salaam na tuachane na nyumba za Tembe, usije na swaga zako za kutuingizia sh 1,000 kwa kila mfuko mmoja wa saruji, hatutakuelewa.”

Habari Zifananazo

Back to top button