Wabunge: Serikali iagize magari yanayotumia gesi
DAR ES SALAAM: KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeishauri serikali kuagiza magari yenye mfumo wa gesi ambao una gharama nafuu.
Hayo yamesemwa Machi 15, 2024 jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa kamati hiyo, David Mathayo wakati wa ziara ya kutembelea vituo viwili vya kuzalisha gesi ambavyo ni Master gas na Taqa Dalbit vilivyopo Dar es salaam.
Kwa upande wake Naibu waziri wa Nishati, Judithi Kapinga amesema amepokea ushauri na maelekezo kutoka kwenye kamati ya bunge na wamejipanga kuongeza vituo 15 vya kujazia gesi vitakamilika ndani ya mwaka huu.
Nae Mkurugenzi wa Shirika la Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame amesema wana mpango wa kununua vituo vya gesi vitano vyenye uwezo wa kuhama kuanzia mwezi Machi hadi Agosti na watavitawanya maeneo mbalimbali.