Wabunge waibana serikali michango mifuko ya jamii

WABUNGE wamewataka Serikali kuhakikisha michango na madeni ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma (PSSSF) zinalipwa.

Rai hiyo imetolewa jana bungeni na Mbunge wa Viti Maalum, Easter Bulaya(Chadema) wakati wa kuchangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/24.

Alisema kuwa kuna mashirika manne hayajapeleka michango takribani Sh bilioni 129 kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ukiwemo mfuko wa PSSSF.

Advertisement

“Mwaka jana nimesema na leo narudia, wakati hizi pesa zinaendelea shilingi bilioni 1.5, fedha za muda mrefu hamjalipa kwenye mifuko iliyoahidiwa na Waziri wa Fedha, atalipa kwa hati fungani zingine hamjatoa.”

“Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tunajua wewe ni mneyenyekevu, tunaomba watumishi watimize wajibu wao, mifuko ya hifadhi ya jamii madeni yalipwe, watumishi fedha zao kwa mujibu wa sheria michango ipelekwe kwenye uwekezaji kuwe na tija ifanyike tathimini ya kina ili hizi fedha za hawa watumishi wa umma ambao ni wastaafu watarajia waje wapate haki zao.”

Bulaya alisema pia Mamlaka ya Serikali za Mitaa 133 hazijapeleka tabribani bilioni 119, maslahi ya mishahara na posho za wafanyakazi hazijalipwa.

“Wakati haya yanaendelea kuna mashirika 8 hayajalipa malimbikizo ya mishahara ya watumishi na madeni mbalimbali takribani shilingi bilioni 5.

8, shilingi bilioni 2.2 ni malimbikizo ya mishahara.”

“Wakati haya yanaendelea kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuna mamlaka 76 hazijalipa Sh milioni 309 za mizigo za wastaafu 223.”

Kuhusu wabadhirifu waliotajwa kwenye ripoti ya CAG, Bulaya alisema yeye binafsi hawafurahii wale wote wanaofanywa ubadhirifu wa fedha za umma.

“Mheshimiwa Rais (Samia) amekerekwa na ubadhirifu, mimi ni nani Easther Bulaya nichukie.

Kama Waziri Mkuu wetu amesikika kwenye ziara zake mbalimbali akikemea ubadhirifu, mimi Easther Bulaya ni nani nimchekee, hasa jicho likiwa limefanya kazi yake.”
“Kwa kumsaidia vivyo hivyo, Rais, kwa kuisadia serikali iweze kuchukua hatua, lazima tuonyeshe kwenye mapungufu hatua zichukuliwe nchi yetu isonge, maendeleo ya taifa yaonekane kwa wananchi wake.”