DODOMA; WABUNGE leo Mei 30,2024 wamepitisha bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka fedha 2024/2025 yenye vipaumbele tisa.
Wizara ya Ujenzi iliomba kuidhinishiwa jumla ya Sh 1,769,296,152,000.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2024/25, ambaapo kati ya fedha hizo Sh 81,407,438,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya wizara na taasisi na Sh 1,687,888,714,000.00 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.