Wabunge washauri mtaji Posta

SERIKALI imeshauri kulisaidia Shirika Posta kupata mtaji na kufuta deni ili kuweka sawa hesabu zake.

Ushauri huo umetolewa leo Mei 19, 2023 na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Bungeni jijini Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti, Mjumbe wa Kamati hiyo, Abubakar Asenga amesema Serikali pia isaidie shirika ili liweze kulipwa madeni yake kutoka taasisi za serikali.

Advertisement

Amesema Serikali kwa kushirikisha wadau muhimu ifanye tathmini ili kuona iwapo inafaa kwa Shirika la Posta kupata kamisheni kutokana na usafirishaji wa mizigo na vipeto unaofanywa na kampuni binafsi nchini.