Wabunge wataka matumizi fedha taslimu yapunguzwe

DODOMA; Wabunge wameitaka Serikali kuhimiza kupunguza matumizi ya fedha taslimu, kwani ni moja ya changamoto ya ukusanyaji kodi.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Juni 4, 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Twaha Mpembenwe, wakati akiwasilisha utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2023/24 na maoni ya kamati kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya mafungu 8 ya wizara pamoja na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi mwaka wa fedha 2024/25.

“Kamati ilibaini kuwa moja ya changamoto katika ukusanyaji wa kodi ni matumizi ya fedha taslimu. Aidha, Serikali imekuwa ikishindwa kufuatilia miamala ya biashara kwa sababu ya malipo kufanyika kwa fedha taslimu.

“Mheshimiwa Spika, Kamati inaishauri Serikali kufanya mabadiliko katika Sheria ya Mifumo ya Malipo Sura ya 437 na Sheria ya Usimamizi wa Kodi Sura 438 na kuanzisha sharti la kufanya malipo kwa njia ya kieletroniki wakati wa kufanya manunuzi ya huduma na bidhaa.

“Aidha, mabadiliko hayo yanaweza kuweka mazingira mahususi yatakayowezesha matumizi ya fedha taslimu.

“Serikali iendelee kutoa elimu kwa wananchi na kuhimiza watoa huduma za kifedha kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kufungua akaunti na kuweka fedha zao kwenye mabenki na kuwahamasisha kuacha kutumia fedha taslimu,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button