Wachangia Sh Mil 350 kutibu magonjwa ya macho

MTWARA: WADAU mkoani Mtwara wamechangia Sh milioni 350 kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wa macho wenye uhitaji.

Akikabidhi kiasi hicho cha fedha, kwa Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanzania inayoratibu matibabu hayo, Mkurungezi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo Kanda ya Pwani, Aidan Komba amesema Tigo imeamua kudhamini taasisi hiyo ili kuhakikisha watanzania wengi wenye matatizo ya macho wanafikiwa.

“Tumedhamini huduma ya kutoa matibabu ya macho kwa sababu tunatambua umuhimu wa kuona hasa kwenye kufanya shughuli mbalimbali za kujitafutia kipato na uchumi,” amesema.

Komba amesema hayo wakati wa uzinduzi wa shughuli ya utoaji wa huduma ya macho bure kwa wakazi wa Mtwara Mikindani na Mitengo ambapo madaktari bingwa kutoka Taasis ya Bilal Muslim Mission Tanzania wamefika kutoa matibabu hayo.

Amesema kupitia pesa hiyo ambayo, Taasis ya Muslim Mission Tanzania wataweza kutoa matibabu kwa wananchi wapatao 4000 kwa Mkoa wa Mtwara.

Mratibu wa Huduma ya Macho Taasis ya Bilal Muslim Mission Tanzania Hassan Dinya amesema taasis hiyo itakaa kwa siku tatu Mtwara ambapo watatoa matibabu kwa Mtwara Mikindani na Mitengo.

Amesema huduma mbalimbali zinatolewa ikiwemo kupewa rufaa kwa matibabu zaidi kwa wananchi watakaokutwa na tatizo lenye kuhitaji matibabu zaidi.

Habari Zifananazo

Back to top button