Wachezaji 12 Chelsea majeruhi
Mambo yanazidi kuwa magumu Chelsea, ambapo mpaka sasa idadi wa wachezaji 12 wa kikosi hicho ni majeruhi.
–
Wachezaji hao ni Reece James nyama za nyuma ya paja, Christopher Nkunku, Wesley Fofana, Carney Chukuemeka, Armando Broja na Moise Caicedo ambao wote wanasumbuliwa na maumivu ya goti.
–
Marc Cucurella, Noni Madueke, Marcus Bettinelli wote wanasumbuliwa na magonjwa mengine, Trevor Chalobah, Benoit Badiashile wanasumbuliwa na maumivu ya paja.
–
Usajili mpya Romeo Lavia pia anasumbuliwa na maumivu ya kisigino.