Wachezaji 12 nje United ikiikabili Bayern
MENEJA wa Manchester United, Erik ten Hag anasem “hajawahi kuanzisha kikosi chake bora zaidi” huku timu yake iliyokumbwa na majeraha ikijiandaa kukabiliana na Bayern Munich michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
–
United itawakosa wachezaji 12 wa kikosi cha kwanza.
–
Wachezaji hao ni Raphael Varane, Mason Mount na Harry Maguire, ambao hawajasafiri kwenda Munich.
–
“Nadhani sikuwahi kuanzisha kikosi bora yote unatakiwa kukabiliana nayo. Napenda hali hizi. Unapaswa kujua nini cha kufanya na kuzingatia mchakato.”
–
Beki Varane na kiungo Mount wote walishiriki mazoezi Carrington Jumanne asubuhi ili kuongeza matumaini ya kurejea kwenye mchezo wa ufunguzi wa Kundi A, ambalo pia linajumuisha Galatasaray ya Uturuki na FC Copenhagen kutoka Denmark.
–
Varane amekosa mechi mbili zilizopita na Mount tatu, huku United wakianza vibaya msimu wa Ligi Kuu, wakipoteza michezo mitatu kati ya mitano ya kwanza.
–
Beki wa kati Maguire pia alifanya mazoezi Jumanne, lakini alipata jeraha ambalo lilimfanya kuwa nje.
–
Ten Hag pia anawakosa washambuliaji Antony na Jadon Sancho, ambao hawafanyi mazoezi na kikosi kwa sasa, pamoja na kiungo wa Uholanzi Donny van de Beek, ambaye hajasajiliwa kwa michezo ya Ulaya.