Wachezaji 30 waitwa kambini Twiga Stars

Wachezaji 30 waitwa kambini Twiga Stars

WACHEZAJI 30 wa timu ya soka ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ wanatarajia kuingia kambini Aprili 2 mwaka huu kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kenya.

Akizungumza na HabariLEO, Kocha Mkuu wa  timu hiyo, Bakari Shime amesema kambi hiyo ni utaratibu uliopo kwenye kalenda yao ya mwaka, lengo ni kuwaweka tayari wachezaji wao kwa mashindano yajayo ya Cecafa.

“Lengo letu ni kukutana angalau mara tatu kwa mwaka, ili kuimarisha viwango vya wachezaji kwa kufanya mazoezi kwa pamoja na kucheza mechi za kirafiki kama tutakayocheza na Kenya Aprili 9 Uwanja wa Benjamin Mkapa,” amesema Shime.

Advertisement

Wachezaji walioitwa ni Najat Abasi, Stumai Abdallah, Happy Hezron, Anastazia Katunzi, Donisia Minja, Jakline Shija na Eto Mlezi , Enekia Kasongo , Julieth Singano , Opa Clement , Aisha Masaka na Diana Lucas.

Wengine ni Fatuma Mwisendi, Zuwena Aziz, Fatuma Issa, Gelwa Yona, Amina Ramadhan, Ester Mayala, Amina Ally, Fumukazi Ally, Emiliana Mdimu, Lucia Mrema, Irene Kisisa, Janeth Christopher, Maimuna Kaimu Zulfa Makau, Husna Mtunda, Protasia Mbunda,  Ester Mabanza na Anatoria Audax.

1 comments

Comments are closed.