MOROGORO: MCHEZAJI wa timu ya Bandari Tanga katika mchezo wa kurusha tufe, Joseph Mwambipilie ameshika nafasi ya kwanza wa kurusha umbali wa mita 9. 80 na kuwazidi wenzake watano walioshiriki mchezo huo kwa upande wa wanaume.
Nafasi ya pili ilinyakuliwa na Mohamed Fadhal kutoka Bandari Tanga aliyerusha umbali wa mita 9.
10 na mshindi wa tatu ni David Mutabuzi kutoka Bandari Dar es Salaam (Dar Port )aliyerusha umbali wa mita 8.64.
Kwa upande wa wanawake, Monica Mlay kutoka Dar Port alichukua nafasi ya kwanza kwa kurusha umbali wa mita 8.30, akifuatiwa na Mary Mwakapasa kutoka Tanga aliyerusha umbali wa mita 7.15 na Fadhila Hamidu kutoka Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), akishika nafasi ya tatu kwa kurusha umbali wa mita 7.01 washiriki pia walikuwa sita .
Kwa uapnde wa kurusha mkuki wanaume , Joseph Robert kutoka Mtwara alishika nafasi ya kwanza kwa kurusha umbali wa mita 41 akifuatiwa na Musa Muhanza kutoka MSCL aliyerusha umbali wa mita 35 na watatu ni Rajab Musa kutoka Makao makuu (HQ) aliyerusha kwa umbali wa mita 34.
20 na washiriki walikuwa sita.
Michezo hiyo ya 17 ya siku nane ilianza Oktoba 23, 2023 inafikia tamati Oktoba 30, 2023 katika Uwanja wa Jamhauri Morogoro ambayo imeshirikisha Wanamichezo takribani 800 kutoka timu Nane za TPA Makao Makuu, Bandari ya Dar es Salaam, Bandari ya Tanga, Bandari Mtwara, Bandari za Maziwa, Shirika la Bandari Zanzibar-ZPC, Kampuni ya Huduma za Meli – MSCL na Timu ya Terminal II (Zamani ikiitwa TICTS).