Wachimbaji migodini hawajaonekana Zambia

MAOFISA nchini Zambia wameshindwa kupata makumi ya wachimbaji haramu wanaoaminika kunaswa baada ya maporomoko ya udongo kwenye mgodi wa shaba Ijumaa.

Ajali hiyo ilitokea katika jimbo la Kaskazini la Copperbelt nchini humo baada ya mvua kubwa kunyesha.

Vikosi vya uokoaji vimekuwa vikivuta maji kutoka kwenye mashimo ya chini ya ardhi kwenye mgodi wa Sesili uliopo Chingola lakini hawakuwapata na wachimbaji hao.

Rais Hakainde Hichilema alisema amesikitishwa na “hali hiyo ya kuhuzunisha”. Makamu wa Rais, Mutale Nalumango alisema tukio lililotokea katika mgodi wa Sesili ni janga.

Habari Zifananazo

Back to top button