Wadaiwa sugu wa maji watangaziwa msamaha

DODOMA: Waziri wa Maji Jumaa Aweso
amewaelekeza watendaji wote wa mamlaka za maji mijini hadi wilayani kusamehe wateja wake madeni.

Aweso ametoa maelekezo hayo leo Machi 26, 2024 mjini Dodoma katika Kikao Kazi kikao kazi cha viongozi na watendaji wa sekta ya maji ikiwa ni pamoja na Menejimenti ya wizara ya Maji, wakurugenzi watendaji wa mamlaka zote za maji pamoja na Mameneja wa mikoa Maji Vijijini RUWASA kwa lengo la kuendelea kukumbushana na kuelezana kwa msisitizo wajibu wa sekta katika kufanikisha utendaji kazi, utoaji huduma na utekelezaji wa miradi ya Maji inayoendelea hapa nchini.

Amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani alipotuma salamu za Kilele cha Wiki ya Maji ameelekeza Mamlaka za Maji kutoa hamasa kwa wateja wake kwa kusamehe na kuondoa faini kwa kipindi cha mwezi mmoja na kusisitiza mteja awajibike tu kulipia sehemu ya deni lake alisia taratibu na kurejeshewa maji huku akiendelea kufurahia huduma ya upatikanaji wa majisafi na salama.

Advertisement

Aidha, Aweso amewataka watendaji wote Mamlaka za Maji na Bodi zake kuwa kipimo cha ufanisi katika kazi kitakua katika maeneo ya kudhibiti upotevu wa maji pamoja na kutochelewesha maunganisho mapya kwa mteja mwenye kutaka huduma ya Maji.