WADAU mkoani Shinyanga wameelezwa kuitambua Programu Jumuishi ya Taifa ya Makuzi,Malezi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT-MMMAM) kupitia nguzo tano zinazo mwezesha mtoto kuwa katika ukuaji timilifu.
Mratibu wa afya ya uzazii,mama,baba na mtoto mkoani Shinyanga Halima Hamis akitoa utambulisho wa Programu ya PJT-MMMAM leo katika kikao cha kamati ya huduma za afya ya misingi ya mkoa kwa ajili ya maandalizi ya kampeni kitaifa ya chanjo dhidi ya magonjwa ya Surua na Rubella, tathimini ya lishe na mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu.
Mratibu Halima Hamis amesema katika nguzo tano lipo eneo la ujifunzaji,lishebora, afya ,malezi yenye mwitikio , ujifunzaji wa awali na ulinzi na usalama.
Hamis amesema mtoto anatakiwa kupatiwa lishe bora na kuwa na afya nzuri kabla na baada ya kuzaliwa na kupewa nafasi ya ujifunzaji katika mazingira yanayo ruhusu kwa usalama zaidi.
Halima amesema katika utafiti uliofanywa mtoto kuanzia umri wa mwaka 0 hadi minane (8) anakuwa na uwezo wa uelewa kupitia hatua hiyo anatakiwa nguzo hizo tano muhimu azipitie bila kupata changamoto yoyote ikiwemo kupatwa na vitendo vya ukatili.
“Mtoto anatakiwa kujengwa kabla ya ubongo wake haujakomaa hivyo ni muhimu apatiwe lishe nzuri akiwa bado tumboni na kuzungumza naye”amesema Hamis.
Hamis amesema mtoto akifanyiwa vitendo vibaya vya ukatili anakuwa navyo moja kwa moja hata katika makuzi yake yana muathiri kisaikolojia.
Katika kikao hicho kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Faustine Mulyutu akiongelea suala la chanjo ya surua Rubella amesema kupitia kampeni hiyo wanatarajia kuwachanja watoto 300,193 na vituo 236 vya kutolea huduma za afya na vituo 123 vya muda vimeandaliwa kwaajili ya kutoa huduma za chanjo.
Mulyutu amesema Kampeni hiyo ina la kuongeza Kinga kwa watoto wote wenye umri wa kuanzia miezi tisa hadi miezi 59.