“Wadau utamaduni wahudumiwe kwa wakati”

KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu amewataka watendaji na watumishi wa taasisi chini ya wizara hiyo kuwahudumia wadau wa sekta ya utamaduni na sanaa kwa wakati ili kuleta tija katika utendaji kazi.

Aliyasema hayo leo, Juni 20, 2023 jijini Dar es Slaaam wakati alipofanya ziara ya kikazi katika taasisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), bodi ya filamu na michezo ya kuigiza Tanzania pamoja na mfuko wa utamaduni na sanaa Tanzania.

“Tuongeze ubunifu zaidi na kurasimisha wafanyabiashara wa kazi za utamaduni na sanaa na wasanii ili kuunga mkono juhudi za serikali katika utoaji wa huduma kwa wadau wa sekta zetu hizi” alisema Yakubu.

Pia, aliongeza kuwa taasisi zote za wizara zina wajibu kutekeleza vipaumbele vya Serikali ikiwemo kuongeza wigo wa wasanii kwenda kufanya kazi za Sanaa nje ya nchi na kutangaza utamaduni na sanaa ya Tanzania na kuongeza ubunifu katika utendaji kazi wao.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x