Wadau wa habari na mipango ya kuipaisha zaidi sekta hiyo

DAR ES SALAAM: Wadau wa habari Nchini wameendelea kuikumbusha Serikali kuhakikisha inavifanyia kazi baadhi ya Vifungu vya Sheria vilivyopo katika Sheria ya huduma ya vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kifungu kinachoipa Serikali Mamlaka ya kuunda Baraza la kusajili Waandishi wa habari badala ya kufanywa na wanataaluma wenyewe wa habari.

Akizungumza katika Mafunzo Maalumu yaliwakutanisha Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Wadau wengine wa kutoka Taasisi mbalimbali Leo Agosti 25, 2023 Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deudatus Balile amewaomba Wadau hao kuendelea kupitia sheria hiyo pamoja na kupaza sauti ili maombi yao yaweze kufanyiwa kazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dk Anna Henga ameishauri Serikali kuona umuhimu wa kurudisha Muswada bungeni ili kufanyike marekebisho hayo kabla ya Uchaguzi Mkuu ili kuondoa malalamiko hayo na Makosa ya Jinai yaliyomo.

Naye Mwanahabari na Wakili wa kujitegemea James Malenga amesema marekebisho yaliyofanywa ni machache ukilinganishwa na wanavyohitaji wana habari ili kuleta ufanisi katika taaluma hiyo muhimu kwa ustawi wa Taifa.

Habari Zifananazo

Back to top button