WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Pindi Chana, amewakaribisha wadau na wapenda michezo wa sekta binafsi wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika shughuli za michezo hususani mchezo wa netiboli.
Waziri Chana ameyasema hayo leo Juni 23, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mashindano ya klabu bingwa ya netiboli katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.
Ametoa wito kwa wadau wengine zikiwemo taasisi kuwekeza pia katika ujenzi wa miundombinu ya kimichezo na kugharamia shughuli za michezo hususani michezo ya wanawake pamoja na watu wenye ulemavu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli (Chaneta), Dk Devota Marwa amesema kuwa wataendelea kuratibu programu mbalimbali za maendeleo ya mchezo huo.