Waeleza mikakati ya kupambana na TB Afrika

ILI kufikia malengo ya kupambana na maradhi ya kifua kikuu na ukimwi katika nchi tisa za Afrika kwa kipindi cha mwaka 2024 hadi 2026, Dola za Marekani bilioni 130.2 zinahitajika.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Health Promotion Tanzania(HDT), Dk Peter Bujari,  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu mchango wa mifuko ya uwekezaji katika magonjwa hayo.

Dk Bujari ameeleza kuwa fedha hizo zitachangia kuendeleza mapambano ya kutokomeza maradhi hayo kwa kujenga mifumo endelevu ya afya na kuimarisha utayari katika kukabiliana na maradhi, hasa katika nchi tisa ikiwemo Tanzania.

Mkurugenzi huyo amesema kwa Afrika nchi za Afrika Kusini, Kenya, Benin, Namibia, Senegal, Lesotho Ivory Coast , Togo na Zimbabwe zimekuwa mstari wa mbele kwenye kuchangia mfuko huo wa kutafuta tiba ya magonjwa hayo.

Mkurugenzihuyo ameeleza kuwa kwa  mwaka 2002, sekta ya afya Tanzania ilichangia Dola za Marekani bilioni 2.6, fedha hizo zimesaidia kupambana na magonjwa ya ukimwi, kifua kikuu na malaria ambapo zaidi ya watu milioni 1.2 walipata huduma za dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi.

Pia zaidi ya watu milioni 8.2 wamepata huduma na kupona malaria, huku zaidi ya watu 84,000 wamepona kifua kikuu na wagonjwa  391 waliobaki wanaendelea na matibabu.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x