Wafanyabiashara 95 kupata uzoefu China

WAFANYABIASHARA  zaidi ya 95 watashiriki maonesho mafunzo ya wajasiliamali katika onesho la  Canton Fair linaloondelea nchini China, kupitia Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania.

Akifafanua zaidi juu ya safari hiyo, Mkurugenzi wa TWCC, Mercy Sila amesema lengo la safari hiyo ni kuwawezesha wajasiliamali hao kupata fulsa za kimataifa, ambapo wataweza kujionea mashine ya viwanda, vipodozi, mavazi, mashne za kilimo au mashine za kutengeneza chakula .

Alisema mategemeo makubwa ya safari hiyo ni kuhakikisha kwamba  wafanyabiashara hao wakirudi watakuwa sio kama sawa na wale waliondoka kwakuwa biashara zao zitakuwa na kuchangia katika kukua kwa uchumi.

“Serikali inatambua na raisi amefungua milango ya biashara nje ya nchi, ametujengea njia ambayo inatusaidia kufanya biashara kwa amani na utulivu kwakuwa ametuonesha njia”

Mjasiliamali Francis Muhokozi alisema safari hiyo kwake ni ya manufaa kubwa, sababu amekuwa na biashara nyingi hivyo akifika huko ataweza kununua kitu moja kwa moja kuliko kumtuma mtu.

Alisema mwanzo alikuwa na fikra za kuagiza kupitia mtandao, lakini amepata fulsa ya kwenda huko basi atapata nafasi ya kuchagua kilichobora zaidi.

Habari Zifananazo

Back to top button