Wafanyabiashara Kariakoo wakubali kufungua maduka

Wafanyabiashara Kariakoo wakubali kufungua maduka

BAADA ya agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kuwataka wafanyabiashara wa soko la Kariakoo kufungua maduka, hatimaye wafanyabiashara hao wamekubali kufanya hivyo.

Mapema leo jioni Majaliwa aliwataka wafanyabiashara hao kuendelea na biashara zao, huku akiahidi kuzungumza nao Mei 17, 2023 ili kusikiliza changamoto zao na namna ya kuzitolea ufumbuzi.

Advertisement

Akizungumza baada ya kupokea agizo hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo, Martin Mbwana amesema wamepokea agizo hilo na kuahidi kuendelea na biashara zao.

Mbwana ameeleza kuwa wamefikia uamuzi wa kukubali baada ya Waziri Mkuu kufika eneo hilo kuzungumza nao kuhusu changamoto zao na kuahidi kuzungumza nao zaidi Mei 17, 2023.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *