Wafanyabiashara kupewa elimu ya usajili
WAFANYABIASHARA wameshauriwa kutembelea banda la wakala wa usajili, biashara na leseni kwa ajili ya kupewa elimu kuhusu usajili wa kampuni na biashara.
Hayo yamesemwa leo na Ofisa Habari wa Wakala wa Usajili Biashara na Leseni (Brela), Gloria Mbilimonywa wakati wa maonesho ya 18 ya Biashara Afrika Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya Furahisha wilayani Ilemela jijini Mwanza.
Amesema Brela katika maonyesho hayo watakuwa wanasajili kampuni pia watafanya usajili wa alama za biashara.
Ameahidi brela itaendelea kuboresha huduma zao ili ziwe kuwa rafiki.
Maonesho hayo yalianza Agosti 25 na yanatarajia kumalizika Septemba 2 mwaka huu.
Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Daniel Machunda alisema Serikali ya mkoa wa Mwanza itaendelea na mipango endelevu ya kuboresha mazingira ya wafanyabiashara ili kuweza kuwavutia wawekezaji wengi zaidi katika mkoa wa Mwanza.