Wafanyabiashara madini kutembelea China

Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki

WAFANYABIASHARA wadogo na wa kati wa madini nchini Tanzania wanatarajia kufanya ziara nchini China Julai 2023, kwa lengo la kutafuta fursa za ushirikiano na wafanyabiashara wa China.

Taarifa iliyotolewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki inasema wakiwa huko wafanyabiashara hao wanatarajiwa kushiriki katika mkutano biashara utakaowapa fursa za kukutana na wawekezaji mbalimbali, kukutatana na kampuni zinazozalisha teknolojia ya bei nafuu kwa ajili ya shughuli za uchimbaji wa madini pamona na kukutana na watu wenye nia ya kununua madini kutoka Tanzania.

Kwa mujibu wa Balozi Kairuki, ziara hiyo inayoratibiwa na kampuni ya Touchroad Group ya China kwa kushirikiana na Shirikisho la Wachimba Madini (FEMATA) pamoja na ubalozi wa Tanzania ilipangwa na kutangazwa mwaka 2019, ambapo ilikuwa ifanyike mwanzoni mwa mwaka 2020, lakini kutokana na janga la Uviko-19 na hatua ambazo China ilizichukua kufunga mipaka yake ziara hiyo haikufanyika.

Advertisement

Kwa taarifa iliyotolewa na Ofisa mwanadamizi wa Ubalozi wa Tanzania, Dk Miraji Usi, Shirika la Ndege la Air Tanzania itafanya safari maalum ya kusafirisha wafanyabiashara hao katika Jimbo la Zhejiang nchini China sambamba na kundi la watalii kutoka Jimbo hilo kwenda Tanzania.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *