BAADHI ya wafanyabiashara wa Soko la Mbagala Rangi Tatu lililoko jijini Dar es Salaam wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro unaoendelea baina yao na Halmashauri ya Wilaya ya Temeke.
Wafanyabiashara hao wameliambia HabariLEO kwamba wao wana fremu na vizimba sokoni hapo tangu miaka 1980 soko hilo likifahamika kama magengeni likiwa ni mali ya mababu zao.
Mwenyekiti wa wajasiriamali hao, Hamis Makeo alisema jitihada mbalimbali zakurejeshwa sokoni hapo zimefanyika pasipo kuzaa matunda.
Halmashauri ya Temeke ililichukua eneo hilo mwaka 2019 na kulifanya kuwa mali ya serikali kama soko rasmi na kulikabidhi kwa watu wengine. Kutokana na urasimishaji huo, watu walioendeleza eneo hilo wanailalamikia halmashauri na kikundi kiitwacho Umoja wa Wafanyabiashara Sokoni Rangitatu (Uwabisora