Wafanyabiashara sokoni Tanga wapo kamili kwa sensa

WAFANYABIASHARA wa soko la Mgandini jijini Tanga, wametakiwa kutoa ushirikiano, ikiwemo taarifa  kamili kwa makarani wa sensa, wanapopita kwenye maeneo yao, ili kuisadia serikali kupanga bajeti zake kama kuboresha miundombinu ya soko hilo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa soko hilo, Athuman Ramadhani, wakati akizungumza na Daily News Digital na kueleza kuwa taarifa sahihi zitaisaidia serikali inapopanga bajeti zake kuwaboreshea soko hilo.

“Kimsingi tunajua umuhimu wa sensa na manufaa yake kwa jamii, hivyo mimi na wafanyabiashara wenzangu, tupo tayari kuhesabiwa na kutoa ushirikiano wa kutosha,” amesema.

Naye mfanyabiashara sokoni hapo,  Ramadhani Shekwavi amesema amejiandaa kikamilifu kuhesabiwa, huku akiwaasa wafanyabiashara wenzake wajiandae kuhesabiwa kwa kuacha taarifa zao kamili nyumbani, ili karani anapofika asikutane na kikwazo chochote.

Mfanyabiashara mwingine wa samaki sokoni hapo, Bakari Abel, amesema kuwa wao kama vijana wapo tayari kuhesabiwa na kuwashauri vijana wengine kulipa umuhimu zoezi hilo litakalosaidia serikali kupanga bajeti za wananchi wake.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x