Wafanyabiashara wamchongea Mwigulu, Kijaji

WAFANYABISHARA wa Kariakoo wamemchongea Waziri wa Viwanda na  Biashara, Ashantu Kijaji na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba kuwa ndio chanzo cha utitiri wa kodi.

Hayo yamesemwa leo Mei 17,2023 Njjuki Shaban mfanyabiashara ambaye alidai kuwa ndio chanzo cha mgomo katika soko la Kariakoo ambao leo umefikia siku ya tatu.

“Mwigulu Nchemba anaibua kodi zisizolipika, anatuita Dodoma kwenye ‘conference’  kwenye majadiliano hata hatujatoa maoni kashapeleka bungeni eti imeshakuwa sheria, anatufanya sisi hatuna akili.”Amesema na kuongeza

“Wewe unataka sh bilioni 100 na kitu kutoka kwa wasafirishaji unatoa kodi  laki nane mpaka milioni mbili na tisini, watu wanaacha magari, sasa kwa vile Waziri Mkuu unatulinda, nataka nikwambie  hiki kiburi cha TRA  kinasababishwa na ‘boss’ wao Mwigulu.

“Kama inafikia mahala Waziri wa fedha anadharau wabunge wanaotuwakilisha atatusikiliza sisi?….;  “Mwigulu yeye ni dokta, yeye mchumi hawezi kuongea na waganga wa kienyeji.”Amesema

Aidha,  amesema wafanyabiashara wamesikitishwa na kauli iliyotolewa bungeni juzi na Waziri wa Viwanda na Biashara Ashantu Kijaji.

“Mama Kijaji anasema Kariakoo haijafungwa, aliyefunga kafunga kwa hiyari yake, je anastaili kuwa kiongozi wetu huyo? Je ni Waziri wetu huyu? alihoji na kushangiliwa kwa nguvu na wafanyabiashara wenzake.

Aidha alimuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuwa ndio mkuu wa mawaziri waangalie upya sheria za kodi kwa watu wa malori kwa kuwa kiwango cha sh milioni 2.7 hakilipiki.

Pia, alitaka mizani zisomane kwa kuwa kumekuwa na utata kutoka mizani moja kwenda mizani mingine.

“Latra nao uwatizame mheshimiwa Waziri Mkuu, mizani Misugusugu ukipima ukifika Makambako inafika tofuati? Kwa nini inakuwa tofauti? alihoji

 

Habari Zifananazo

Back to top button